RAIS KIKWETE
HAYA NI MAONI YA WANANCHI KWENDA KWA MHE JAKAYA KIKWETE KUPITIA MTANDAO WA FACEBOOK JINSI WATU WANAVYOENDELEA KULIONGELEA SWALA LA ESCROW
Hili shinikizo la kumtaka Rais achukue hatua za haraka kuwawajibisha
watendaji wake linanipa mashaka, linanifanya nianze kuamini yale
yanayosemwa kwamba kuna vita binafsi zimeingizwa kwenye sakata la
ESCROW, ripoti imekabidhiwa kwa Rais, kuna vyombo vimepewa jukumu la
kuchunguza baadhi ya mambo kisha vitoe majibu na hatua zichukuliwe,
haraka ya nini? Mbona wengine walipewa muda wa kuchunguza na kufuatilia
kwanini wengine nao wasipewe muda?
Mhe. Rais, tunakuomba ufanye maamuzi haraka juu ya waliohusika ama moja
kwa moja, ama kwa makosa ya kiuongozi na maadili, katika hili sakata la
ESCROW, kabla wananchi hatujaamua kufanya maamuzi halafu na liwalo na
liwe, maana hii inamaanisha hivi sasa tunasubiri hili lipoe halafu
liibuke lingine, hatutaki upinzani usio na tija, sisi ni wananchi
tunaoumia na maisha ya kila siku, wewe hapo ikulu hata soksi hujui kuwa
imeisha, anayejua ni mwengine, wewe ni kuweka miguu juu tu.
Tafadhali sana
Mheshimiwa, tunza heshima yako kwa kufanya maamuzi magumu juu ya hili.
Hebu ona, umeondoka juzijuzi tu kwamba unaumwa, umeenda kutibiwa
marekani, umerudi ukaanza kujibalaguza kwa kuwasifia madakitari wa
marekani namna wanavyofanya kazi yao kwa weledi mkubwa na kwa taaluma ya
juu kabisa, kutuaminisha kuwa Tanzania madakitari wetu bado sana, na
elimu yetu itasubiri sana. Ukaendelea kutuzuga na stori za kuhusu
ugonjwa wa tezi dume, sawa, tumekaa kimya, sasa umerudi na ni kama wiki
sasa imeyoyoma, umekaa kimya, tuamini nini? ulikimbia ile skendo kwenda
marekani kusubiri iishe ndo urudi? please, tunakusubiri, na utuambie
tukupe siku ngapi ili ufanye maamuzi hayo haraka iwezekanavyo.
Na mwananchi mtiifu.
Ukimya wa Rais Kikwete ktk kutekeleza mapendekezo ya bunge kunanifanya
niamini habari zilizoenea kuwa familia yake (JK) ilihusika na wizi wa
fedha za Escrow.!
ESCROW kuna siri kubwa kati ya rais kikwete na James Rugemalira na seth
wamiliki wa IPTL na PAP kitendo kinachomfanya rais kushindwa kuyafanyia
kazi maamuzi ya bunge.
kuna taarifa kuwa mmoja wa wanafamilia wa rais amechukua bilion 5 pesa
za ESCROW kwa hiyo James Rugemalira na Seth Singh wamekuwa ndio washauli
wa rais kikwete kuhusu suala hili na kikwete anaufanyia kazi ushauri wa
wezi hawa badala ya ushauli wa bunge kwa kuwa anajua moja ya familia
yake wanahusika.kuna mawasiliano ya karibu kwanjia ya imeil na simu kati ya rais na hawa wezi wa ESCROW.
hivyo basi na James Rugemalira ndio waliochukua nafasi ya bunge
kuishauri serikali na rais anaufanyia kazi kwa maana hiyo bunge halina
kazi tena kwa kuwa serikali haifanyii kazi tena ushauri wa bunge na ndio
maana ata rais umeona yuko kimya tangu bunge liazimie wezi wa ESCROW
wachukuliwe hatua pamoja na kwamba nchi wahisani wamegoma kutoa misaada
kwa sababu ya wezi hawa.
tusikubali James Rugemalira na Seth Singh wawe ndio wawe washauri wa
serikali badala ya bunge,yani fisi awe mshauri wa mwenye bucha?
watanzania mpaka sasa tusitegemee rais kuufanyia kazi ushauri wa bunge
kwa kuwa amelidharau hivyo sisi wananchi wabunge na viongozi wa vyama
vya upinzani kumlazimisha rais aufanyie kazi ushauri wa bunge .
Nadhani JK akisikiliza wimbo huu anaweza kuchukua maamuzi ya wale jamaa wa Escrow.
"Waite Waite ite ite, wakalishe chini kwanza, watoe hofu kwanza, wambie wao hawamo japo nao walikula" Mrisho Mpoto.
Wakati akitoa mchango wake bungeni mh Tundu Lissu bungeni kuhusiana na
escrowsaga alijaribu kuhusisha historian ya hili sakata lilivyoanza na
historian ya kiuongozi ya mtu aliyemtaja kama kanali jakaya mrisho
kikwete ambaye ndiye Rais wa Tanzania. Ingawa wabunge wenzie hawakupenda
bado tena mbunge David Kafulila amerudia kusema familia ya Rais
inahusika kwenye wizi wa fedha za escrow. Huenda tuhuma hizi zisiwe za
kweli lakini ukimya wa Rais ktk hili na kuchelewa kwake kutekeleza
maazimio ya bunge kunaleta maswali akilini mwangu juu ya kutohusika kwa
Rais. Nikirejea mchango wa mtoto wa Rais bungeni mh Ridhiwani Kikwete
kuwa hela za escrow siyo za serikali naishiwa maneno ya kuandika. Bofya hapa kwa undani zaidi
0 comments :
Post a Comment