Dodoma, M/kiti wa chama cha demokrasia na maendeleo tawi la UDOM (CHADEMA UDOM) Mh. ANDREA MGAYA ajiuzulu nafasi yake ya uongozi na kutokuendelea tena kuwa kiongozi ndani ya chama, alifikia maamuzi hayo baada ya kutuhumiwa kuwa ameua chama ndani ya chuo kikuu cha Dodoma.
Baada ya maamuzi hayo Mh mgaya alitoa maelezo yake kama alivyo eleza hapa
Kwanza nakanusha kuwa chama hakifa, wala kupoa ndani ya chuo hiki, Ila muamuko umepungua ndani ya wanachama ndani ya chuo hiki kutokana na sababu zifuatazo
· Kuna na ushirikiano hafifu na ngazi zote za uongozi wa chama yaani wilaya, mkoa, kanda, pamoja taifa
· viongozi kuendelea kutoa lawama kwa uongozi ndani ya chama,
· kuwatuwatumia wanachama kwa masilahi ya chama na wanapopata matitizo chama hukaa pempeni au hujitenga,
· viongozi wa chama waliosimamishwa masomo kuulamu uongozi uliopo wakati umeshiki kwa kiasi kikubwa kurudi kwao kwa michango mbalimbali.
· pamoja na CHADEMA ngazi ya juu kutokuona umuhimu wa hadhina ya vyuo vikuu kwa takribani miaka miwili bila kutoa mafunzo yeyote kwa uongozi ulioshikilia matawi ya vyuo vikuu.
· Kutothamini mchango wa uongozi uliopo
Mwisho nawashukuru wanachama wa CHADEMA tawi la UDOM kwa ushirikiano wenu.
0 comments :
Post a Comment