Vijana wakiwa kwenye matembezi ya Uzalendo yalioratibiwa na Umoja wa Vijana wa CCM katika kuadhimisha miaka 50 ya Muungano ambapo vijana hao walianzia matembezi kutoka ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Temeke mpaka kwenye viwanja vya sabasaba na kulakiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete.
Vijana wakionyesha uzalendo kwa kuonyesha skafu zao zenye jina la Tanzania
Ujumbe maridhawa ambao ndio gumzo la mjni kwa sasa.
Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam Ndugu Ramadhani Madabida muda mchache kabla ya kupokea matembezi ya Uzalendo yaliofanywa na vijana mbali mbali .
Mwenyekiti wa UVCCM Ndugu Sadifa Juma Khamis akienda kukabidhi bendera ya Taifa kwa Dk Jakaya Mrisho Kikwete .
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ameshikilia picha ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage huku Rais wa Mapinduzi ya Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiwa ameshikilia picha ya Rais wa kwanza wa Zanzibar Sheikh Abeid Amani Karume baada ya kuzipokea kutoka kwa vijana waliofanya matembezi ya Uzalendo.
0 comments :
Post a Comment