Pata Habari Motomoto za Nje na Ndani ya Nchi kwa njia ya E-mail, Andika E-mail yako hapo chini.


Home » » Ndimi zilizojeruhi ndani ya Bunge Maalumu Dodoma, soma hapa kufahamu hizo kauli

Ndimi zilizojeruhi ndani ya Bunge Maalumu Dodoma, soma hapa kufahamu hizo kauli



Dodoma. Wakati mjadala kuhusu sura ya kwanza na sita kwenye Bunge Maalumu ukielekea ukingoni, baadhi ya wajumbe wametoleana kauli ambazo zimesababisha kutoelewana.


Kiini cha hayo ni aina ya muundo wa Muungano unaotakiwa kuwekwa kwenye Katiba Mpya, suala ambalo wajumbe badala ya kulijadili kwa hoja, wakaishia kushambuliana kwa maneno.


Kwa muda mrefu hali haikuwa shwari, kwani dakika 10 zilizotengwa kwa ajili ya mjumbe kuchangia mjadala, wengi walizitumia kumaliza hasira dhidi ya wenzao au kuponda mchango uliotolewa awali na mjumbe mwingine.


Hebu tuone mifano ya kauli zilizoacha majeraha bungeni hivi karibuni.


Kauli ya Lukuvi


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Sera Uratibu na Bunge, William Lukuvi alisema Chama cha Wananchi (CUF) ni sehemu ya kikundi cha Uamsho kinachoisumbua Serikali ya Zanzibar.


Lukuvi akaenda mbali zaidi na kusema Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharifu Hamad, ni mchochezi ambaye amemtuhumu Rais Jakaya Kikwete kuvuruga Muungano na kudai anastahili kupelekwa katika Mahakama ya Uhalifu wa Makosa ya Jinai The Hague - Uholanzi.


Kauli hii inaweza kuonekana kama njia ya kuzuia wananchi wasikiamini Chama cha CUF katika mchakato wa Katiba Mpya.


Profesa Ibrahim Lipumba


Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba akihitimisha hotuba kwa mujibu wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), akalifananisha Bunge Maalumu na kundi la Intarahamwe.


Kundi hilo ni lile lililoendesha mauaji ya kimbari nchini Rwanda, mwaka 1994.


Felix Mkosamali endeleaa

0 comments :

Post a Comment

 

Copyright © 2013. THE WORLD OF TODAY - Haki zote zimehifadhiwa
Template Modify by World of Today TEAM
Proudly powered by Blogger