Dar es Salaam. Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ametoa ruksa kwa wanachama wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kufanya mikutano yao nchi nzima.
Pinda alizungumza jana wakati akifunga maonyesho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, alisema yaliyotokea bungeni yanaweza kumalizika kwa kukaa meza moja ya majadiliano.
“Yale mambo ya bungeni yanaweza kumalizika na tukaendelea kama ambavyo ilikuwa katika majadiliano ya kutengeneza kanuni. Tulikuwa tukishindana kwa kukaa meza moja na kumalizana, kisha tunaendelea sasa hili tumeshindwa nini?” alihoji Pinda
Alisema: “Walitoka bungeni na kusema watazunguka nchi nzima, nasema wazunguke tu kuwaeleza wananchi na sisi hatutashindwa kuzunguka kwani hoja tunazo.”
Waziri Mkuu Pinda alitumia nafasi hiyo kuelezea kauli aliyoitoa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi kwenye Kanisa la Methodist kwamba hoja ya serikali tatu ikipita inaweza kulifanya jeshi kuchukua madaraka.
Alisema nilimpigia simu nikamweleza: “Rudi mara moja ueleze kilichotokea huko na nafikiri mlimsikia alichokisema.”
Lukuvi akitoa ufafanuzi bungeni bila ya kuwapo kwa Ukawa alisema: “Nayasema yote haya kwa kuwa naamini huo ndio msimamo wangu na utakuwa msimamo ambao wakati wote utaendelea kuwa hivyo na ninawataka ndugu zangu kuacha unafiki.”
Kutokana na kauli hizo, Ukawa inayoundwa na vyama vya Chadema, CUF, DP na NCCR-Mageuzi na wajumbe 25 kutoka kundi la 201 walitoka bungeni Jumatano wiki hii na kuahidi kuzunguka nchi nzima kufanya mikutano ya hadhara kuwaleza wananchi kilichotokea.chanzo mwananchi bofya hapa
0 comments :
Post a Comment