WAZIRI mmoja katika Baraza la Mawaziri la Rais Jakaya Kikwete, mwenye kuongoza moja kati ya wizara nyeti nchini (jina linahifadhiwa) amepanga hujuma dhidi ya wizara yake kwa kushirikiana na baadhi ya wabunge, ili hatimaye bajeti ya wizara hiyo ikwamishwe bungeni, Raia Mwema limeelezwa.
Waziri huyo ambaye amekuwa katika mgogoro na baadhi ya watendaji waandamizi wa wizara hiyo, kiasi cha mgogoro huo kuingiliwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue hivi karibuni, anadaiwa kushirikiana na baadhi ya wabunge vinara ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kufanikisha mpango huo.
Wabunge hao (majina yanahifadhiwa kwa sasa) ambao wamekuwa vinara katika kuzichachafya wizara mbalimbali ni kutoka mikoa ya Mara (mmoja), Shinyanga (mmoja), Tanga (mmoja) na Arusha (mmoja), taarifa zikieleza kwamba wamekwishakupewa ‘fungu’ na maelekezo ya kufanya wakiwa bungeni, pindi bajeti ya wizara hiyo ambayo Waziri wake wa awali aling’olewa kwa shinikizo la Bunge, Desemba mwaka jana, pamoja na mawaziri wengine kadhaa.
Mawaziri waliong’olewa Desemba mwaka jana, kutokana na shinikizo la Bunge ambalo msingi wake ni utekelezaji wa Operesheni Tokomeza Ujangili ni pamoja Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Hamis Kagasheki, Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi, Waziri wa Maendeleo ya Mifugo, Dk. Mathayo David Mathayo na Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha.
Ni hujuma dhidi ya wizara, Ikulu
Msingi wa hujuma hizo za Waziri huyo unatajwa kutokana na uamuzi wake alioutangaza Februari 24, mwaka huu wa kuwaondoa kazini baadhi ya watendaji wakuu katika wizara anayoiongoza (majina yanahifadhiwa), kinyume cha utaratibu.
Hata hivyo, uamuzi wake huo haukuungwa mkono na Ikulu, kupitia kwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue ambaye alitaka taratibu za utumishi wa umma zifuatwe katika suala hilo na hatimaye, watendaji hao kurejeshwa katika nyadhifa zao za awali.
Kutokana na hali hiyo, taarifa kuhusu njama hizo zinabainisha kwamba waziri huyo ameungana na baadhi ya wabunge hao vinara bungeni ili kuzuia kupitishwa kwa bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2014/2015, kwa hoja kwamba uamuzi wa kuwarudisha kwenye nyadhifa zao watendaji hao waandamizi aliowang’oa awali, ni kudharau maazimio ya Bunge la Jamhuri.
“Kuna fedha zimesambazwa kwa baadhi ya wabunge kufanya kazi hiyo ya kukwamisha bajeti ya wizara (inatajwa jina), wanataka kuikomoa Ikulu kwa kumwingilia waziri na kutengua uamuzi wake,” anaeleza mtoa habari wetu.
Vigogo wa Bunge wahusika
Kwa mujibu wa mtoa taarifa wetu, hujuma hizo zinawahusisha vigogo wawili wa Bunge ambao ni sehemu ya Kamati ya Uongozi ya Bunge. Vigogo hao watatu wanaingia katika Kamati ya Uongozi ya Bunge kutokana na nyadhifa walizonazo kwa sasa.
Wawili kati ya viongozi hao wanaingia katika Kamati ya Uongozi ya Bunge kutokana na nafasi zao kwenye kamati za kisekta na mwenzao mwingine yumo kwenye kamati hiyo kutokana na kuwa msaidizi wa Spika, Anne Makinda. Majina yao yanahifadhiwa angalau kwa sasa.
Taarifa zaidi zinabainisha kwamba, kwa muda sasa tangu Waziri huyo ateuliwe kuongoza wizara hiyo, amekuwa karibu mno na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Sekta yenye uhusiano na Wizara anayoongoza, wakisafiri pamoja nje ya nchi, huku safari yao mojawapo waliyofanya wiki kadhaa zilizopita, kwa kutumia fedha za wizara, ikizua utata.
Waziri na mwenyekiti huyo walikwenda kushiriki moja ya mikutano ya sekta wanayoongoza jijini London, Uingereza lakini katika hali ya kushangaza, Mwenyekiti huyo wa kamati aliishia kubaki hotelini siku zote za mkutano, huku akiwa amelipwa fedha za wizara hiyo inayoongozwa na waziri huyo chanzo. RAIA MWEMA

0 comments :
Post a Comment