Mwenyekiti mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Profesa
Ibrahim Lipumba akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari, Dar
es Salaam jana, akiwa na wenyeviti wenzake wa umoja huo, Freeman Mbowe
(kushoto) na James Mbatia (wa pili kulia). Kulia ni Katibu Mkuu wa
Chadema, Dk Willibrod Slaa. Picha na Michael Matemanga
Ni katika kikao cha maridhiano chini ya Msajili wa Vyama vya Siasa
Ni katika kikao cha maridhiano chini ya Msajili wa Vyama vya Siasa
Dar es Salaam. Kete ya mwisho ya
kuamua iwapo wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) watarejea
katika Bunge la Katiba au la itachezwa leo katika kikao cha maridhiano
baina ya umoja huo na CCM, chini ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji
Francis Mutungi.
Kikao hicho kinafanyika siku nne kabla Bunge hilo
kuendelea na vikao vyake Jumanne ijayo licha ya msimamo wa Ukawa wa
kuendelea kuvisusia.
Kikao hicho kinachovikutanisha vyama vya
NCCR-Mageuzi, Chadema, CUF na CCM ni cha mwisho baada ya kile cha kwanza
kilichofanyika wiki moja iliyopita kumalizika bila mwafaka wowote.
Akizungumza na waandishi wa habari jana akiwa na
wenyeviti wenzake, James Mbatia (NCCR-Mageuzi) na Profesa Ibrahim
Lipumba (CUF), Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema hadi jana
msimamo wao ni kutohudhuria vikao vya Bunge hilo labda ikitokea miujiza
katika kikao cha leo.
Mbowe alisema ni miujiza kwa sababu kwa madai ya
Ukawa, ni lazima mjadala huo ujikite kwenye Rasimu ya Katiba, ambayo
imebeba mapendekezo ya wananchi na kutaka wajumbe wenzao, hasa kutoka
CCM, kuacha kujenga hoja kwa kutumia kejeli, matusi na mizaha ambayo si
rahisi wenzao kuyakubali.
Moja ya ajenda ya kikao hicho ambacho leo kitakuwa
na wajumbe 20 kutoka kila chama, ni kuwashawishi Ukawa kurejea bungeni
ili kuendelea na mchakato wa Katiba Mpya.
Ukawa walisusia vikao vya Bunge la Katiba hilo
Aprili 16 wakipinga kubadilishwa Rasimu ya Katiba na wajumbe wa CCM kwa
maelezo kuwa ni kinyume na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.
Mbowe alisema ni jambo la kushangaza kuona Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda na Mwenyekiti wa Bunge la Katiba, Samuel Sitta
wakitoa kauli za kuwashutumu Ukawa wakati wakijua wazi kuwa kuna
mazungumzo kati ya vyama vya siasa na Jaji Mutungi vinaendelea.
Juzi pia, Baraza Kuu la Waislamu Tanzania
(Bakwata), liliisihi Ukawa kurudi bungeni ili kukamilisha mchakato wa
kupata Katiba Mpya, lakini likasema mjadala huo uzingatie Rasimu ya
Katiba.
“Hata viongozi wa dini nao wametoa matamko
wakitaka Ukawa turejee bungeni, tunashukuru maoni yao. Ila wanatakiwa
kujua sababu zilizotufanya mpaka tukasusia. Wanatakiwa kuwaonya CCM
wanaokwenda kinyume na mchakato huo,” alisema Mbowe na kuongeza:
“Wakati tupo katika mazungumzo, Sitta anaanzisha
kikao chake na kutoa tamko kuwa Bunge litaendelea wakati akijua Ukawa
wapo katika kikao pamoja na viongozi wa chama chake cha CCM. Kauli hizi
zinazokosa umoja zinaonyesha Serikali na timu nzima haiko tayari
kutafuta mwafaka wa suala hili. endelea
0 comments :
Post a Comment