Prince William wa Uingereza anakutana Jumatatu na Rais wa Marekani
Barack Obama huko White house. Mfalme huyo wa baadae anatarajiwa
kuzungumza na Rais kuhusu biashara haramu ya wanyama pori.
Baada ya mkutano wake na bwana Obama, William atatoa hotuba kwenye
mkutano wa Benki ya Dunia wa International Corruption Hunters Alliance
mjini Washington.
Anatarajiwa kusema biashara haramu ya pembe za ndovu, pembe za faru
na sehemu nyingine za mnyama ni “moja ya chanzo kikuu cha rushwa na
uhalifu duniani hii leo” na wale wanaoangalia “njia nyingine au
wanatumia mapato haramu kwa uhalifu huu lazima wawajibishwe”.
Prince William pia ataelezea kwamba baadhi ya viungo vya mnyama vina thamani kubwa zaidi ya uzito wao katika dhahabu.
William, mke wake Kate na kaka yake Prince Harry ni waanzilishi wa taasisi ya hisari ya Britains United for Wildlife.
Familia hiyo maarufu ya malkia wa Uingereza iliwasili New York,
Marekani jumapili kwa ziara ya siku tatu nchini Marekani. Ni mara yao ya
kwanza kwa familia hiyo kufika jiji la New York
0 comments :
Post a Comment