Kamati tendaji tawi la UDOM.
kamati tendaji tawi la UDOM inapenda kuwataarifu wanachama na wapenzi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwamba;-
kukanusha taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii juu ya Ndg Andrea Mgaya kujiuzulu nyazifa ya uenyekiti wa tawi la UDOM.
ufafanuzi juu ya taarifa hii ni kwamba tar.4/4/2014 kamati tendaji ilikutana kujadili mwenendo wa chama katika tawi la UDOM. katika kikao hicho kwa kuzingatia katiba ya chama ilimsimamisha Ndg mtajwa hapo juu kwa makosa yafuatayo.
- kukiuka taratibu za kiuongozi, yaani kutoa malalamiko juu ya chama na viongozi wa kitaifa nje ya vikao halali vya chama. Rejea katiba ya chama sura ya 9 ibara ya 3.0 kifungu kidogo cha (c)
- utendaji ndani ya tawi kuwa mbovu hasa nafasi yake kama mwenyekiti wa tawi, kutokana na utendaji wake kuwa duni hivyo kamati tendaji ililidhia kumsimamisha ili kunusuru hali ya chama ndani ya tawi la UDOM. kwa kuzingatia katiba ya chama sura ya 7 ibara ya 7.7.1 kifungu kidogo cha (i) na (v) kama mwenyekiti alishindwa kuendesha na kusimamia vikao halali kwa mjibu wa katiba.
- masuala mengine ni juu ya kuhusishwa kwake na kuwa na mawasiliano ya karibu na viongozi wa magamba yaani CCM. hivyo kuratibu mipango yote ya kuua chama cha kiukombozi.
imetolewa na katibu mwenezi tawi la UDOM
0 comments :
Post a Comment