Pata Habari Motomoto za Nje na Ndani ya Nchi kwa njia ya E-mail, Andika E-mail yako hapo chini.


Home » » Mkasa wa mwenyekiti wa CCM aliyeliwa na mamba

Mkasa wa mwenyekiti wa CCM aliyeliwa na mamba

Mvua inaweza kuwa neema pale inaponyesha kwa wastani, lakini ikawa karaha pale inapokuwa kubwa, hasa kwa watu wanaoishi mabondeni au kandokando ya mito.


Mikoa mingi nchini imepata adha ya mafuriko kutokana na mvua zilizoanza kunyesha mwezi uliopita. Lakini kwa wakazi wa vijiji vilivyopo kandokando ya Mto Rufiji, mvua zimewaletea wageni hatari katika maeneo yao.


Wageni hawa ni viumbe hatari; ni mamba waliowageuza wenyeji wao kuwa kitoweo na kuwafanya waishi kwa wasiwasi wakihofia usalama wao.


Wakazi hawa wanashindwa kuendelea na maisha yao kama kawaida, ikiwemo shughuli za kilimo ambazo huzifanyia ng’ambo au pembezoni mwa mto huo.


Kwa muda mrefu sasa mnyama huyo amekuwa tishio kwa wakazi wa Wilaya ya Rufiji. Wanyama hao wengi huishi katika mabwawa yaliyopo katika Hifadhi ya Selous, lakini mvua inaponyesha na maji kujaa mtoni, mamba hurahisishiwa kazi ya kuwinda binadamu.


Wakazi wa vijiji vya Utete, Chemchem, Mkongo, Ngorongo, Nyaminywili, Mloka na Mwaseni hujishughulisha na kilimo cha mazao ya mahindi, mpunga, ndizi na matikitimaji kando ya mto huo.


Wengi wao hulazimika kuvuka mto huo ili kwenda ng’ambo ya pili kulima, au kuwinda ndege na usafiri wao mkubwa ni mitumbwi ambayo siyo salama katika kipindi hiki.


Hivi karibuni, mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi tawi la Lumumba katika kijiji cha Kilimani Mashariki, Saidi Simba (60) aliliwa na mamba wakati akivuka mto huo.


Akiwa na mwanawe wa kiume, Seif Saidi (5) mtumbwi waliokuwa wakisafiria ulijaa maji na kumlazimu kushuka ili ayaondoe.


Aliposhuka tu alipokelewa na mamba ambaye alimzamisha na kutoweka naye huku mtoto wake akibaki na taharuki na kulazimika kupiga kelele kuomba msaada.


Ofisa mtendaji wa Kijiji cha Kilimani Mashariki, Masudi Mminge anasema kuwa katika eneo hilo, mamba huweka makazi hasa wakati wa mvua.


Anasema tatizo la wanyama hao ni kubwa katika kijiji chake na vijiji vya jirani, hasa katika kipindi cha masika. endelea.....

0 comments :

Post a Comment

 

Copyright © 2013. THE WORLD OF TODAY - Haki zote zimehifadhiwa
Template Modify by World of Today TEAM
Proudly powered by Blogger