Michael Silanda ( 26 ) mkazi wa kijiji cha Ibindi, tarafa ya Nsimbo wilaya ya Mlele mkoani Katavi amefariki dunia baada ya kunywa pombe ( Viroba ) aina ya Zed kupita kiasi bila kula chakula….
Kamanda wa polisi mkoani Katavi,Kamishna Msaidizi Mwandamizi,Dhahiri Kidavashari amesema tukio hilo limetokea wiki iliyopita majira ya saa sita usiku kijijini hapo…..
Alisema siku ya tukio marehemu baada ya kuamka asubuhi nyumbani kwake hapo majira ya saa tano asubuhi alielekea kwenye baa ambayo ilikuwa ikiuza vinywaji vya aina mbalimbali zikiwemo pombe kali….
Alifafanua kuwa,baada ya kufika kwenye baa hiyo aliwakuta baadhi ya wanakijiji wenzake wakiwa wanakunywa pombe za aina mbalimbali hali ambayo ilimfanya marehemu aweze kujumuika nao kwa kuagiza pombe aina ya Zed…
Alisema Michael aliendelea kunywa viroba kuanzia muda huo kwenye baa hiyo bila kula kitu chochote hadi majira ya saa sita usiku alipoamua kurudi nyumbani kwake huku akiwa amelewa pombe kupita kiasi….
Baada ya kufika nyumbani kwake aliingia ndani ya nyumba yake na kulala bila kula chakula cha aina yoyote na siku iliyofuata majira ya saa mbili asubuhi ndipo walipomkuta Michael akiwa amefariki huku akiwa amelala kitandani kwake,….. Kamanda Kidavashari alisema uchunguzi wa awali uliofanywa kuhusiana na tukio hilo umebaini kuwa kifo hicho kimesababishwa na marehemu kunywa pombe nyingi kupita kiasi bila kula chakula…gumzo

0 comments :
Post a Comment