Tanga.
Watu watatu wa familia moja, wakazi wa Kijiji cha Kwasunga wilayani
Handeni wamekufa baada ya kula futari ya mihogo inayosadikiwa kuwa na
sumu.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, kamanda wa polisi wa Mkoa wa Tanga, Constantine Massawe alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 1:00 usiku eneo la Kwasunga Handeni na maiti zimehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Handeni. (FS)
Kamanda
Massawe alisema kwa mujibu wa wazazi wa watoto hao, walikula futari hiyo
na baada ya kumaliza, walianza kujihisi vibaya sambamba na kuishiwa
nguvu na alianza kuanguka mmoja baada ya mwingine.
Kamanda huyo aliwataka wote walio katika mfungo kuichunguza mihogo wanayoinunua kwa ajili ya matumizi ya futari kwani baadhi haifai kuliwa na binadamu.
0 comments :
Post a Comment