Kumetokea ufyatulianaji mkali wa risasi katika kambi ya kijeshi katika mji mkuu wa Kinshasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Taarifa
zinasema kuwa raia wameondolewa katika eneo hilo na haijafahamika
makabiliano hayo yaliyotokea katika kambi ya wanajeshi wa kumlinda rais
yametokana na nini.
Wadadisi wa
mambo wanahisi kwamba kisa hiki huenda kikazusha utata tena kati ya
Congo Kinshasa na Congo Brazzaville kwa vile shambulio lilitokea karibu
na mpaka kati ya nchi hizo mbili.
Taarifa
kutoka kwa serikali zinasema kuwa wavamizi walijaribu kupenyeza katika
kambi ya kijeshi ya Camp Tshatshi na makabiliano yalizuka kwa zaidi ya
dakika 30 hivi.
Jamhuri hiyo
ya Kidemokrasia ya Congo imesakamwa na vita kwa kipindi kirefu sasa na
hata rais aliyepo madarakani kwa sasa Joseph Kabila alichukua mamlaka
baada ya kuuawa kwa babake Laurent Kabila mwaka wa , 2001.
Raiya walihamishwa kutoka maeneo yaliyoko karibu na uwanja wa ndege ulifungwa wakati wa shambulizi hilo.
Serikali bado haijamtaja nani aliyeishambulia .
Hii sio mara ya kwanza kwa Camp Tshatshi kushambuliwa mwaka uliyopita kami hiyo ilishambuliwa tena na wakati huo wafuasi wa dini ya ya kikristo ya dhehebu linaloongozwa na Paul Joseph Mukungubila walilaumiwa
0 comments :
Post a Comment