Watu
wasiojulikana wamemuua Mwalimu Dionizi Ng’wandu wa Shule ya Sekondari
Kagemu iliyopo nje kidogo ya Mji wa Bukoba na kumkata mguu mtu mwingine
wakati wakifanya maombi kanisani.
Tukio
hilo lilitokea usiku wa kuamkia Ijumaa wakati mwalimu huyo pamoja na
mwenzake aliyetambuliwa kwa jina moja la Themistocles ambao ni waumini
wa Kanisa la Pentecostal Asemblies of God (PAG) walipoamua kuendelea na
mkesha baada ya wenzao kuondoka.
Kwa
mujibu wa Mchungaji wa kanisa hilo, Faustin Joseph saa chache kabla ya
mauaji hayo walikuwa wakifanya maombi wakiwa kundi la watu wanne na
ilipofika saa tano usiku waliondoka na kuwaacha wenzao wawili.
‘’Tunao utaratibu wa kufanya maombi, ilipofika saa tano usiku mimi na mwenzangu mmoja tuliondoka na kuwaacha wenzetu wawili na ilipofika saa nane usiku nilipigiwa simu na majirani kuwa kuna mauaji yamefanyika kanisani,’’ alisema mchungaji huyo.
Pia,
mchungaji huyo alibainisha kuwa wauaji hao hawakuchukua mali yoyote na
kuwa siku chache kabla ya mauaji hayo watu wasiojulikana walivamia
kanisani hapo na kuiba viti pamoja na vitambaa jambo alilosema
liliwafanya waone umuhimu wa kuchukua tahadhari.
Akizungumzia
mauaji hayo Mwenyekiti wa Makanisa ya Kipentekoste mkoani Kagera,
Crorwad Edward alisema tukio hilo limewaletea mshtuko na kuwa
wanajiandaa kutoa tamko kwa kuwa pia yaliwahi kuwepo matukio ya kuchoma
moto makanisa.
Akithibitisha
kuwapo kwa mauaji hayo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Henry
Mwaibambe alisema muumini huyo ni Mwalimu wa Sekondari ya Kagemu na kuwa
majeruhi aliyekatwa mguu amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa.
Pia,
alisema kuwa tayari wameanza uchunguzi kuhusiana na mauaji hayo
aliyosema yamefanywa na watu wanne na kuwa mtuhumiwa mmoja amekamatwa
kwa ajili ya mahojiano na kuahidi kutoa taarifa zaidi baadaye. gumzo la jiji
0 comments :
Post a Comment