Pata Habari Motomoto za Nje na Ndani ya Nchi kwa njia ya E-mail, Andika E-mail yako hapo chini.


Home » » Mjumbe NCCR awatesa vigogo

Mjumbe NCCR awatesa vigogo



Kutokana na alichofanyiwa kwa kupigiwa kura bila huku akiwa hajafanya hivyo tumemwandikia barua IGP tukimwomba amwekee ulinzi (Hamis) kwani kwa siasa za Pemba (anakoishi Hamis) wanaweza kumdhuru.”PICHA|MAKTABA





Dar es Salaam. Siku moja baada ya Makamu Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi- Zanzibar, Haji Ambar Hamis kutoa tuhuma za ‘kupigishwa’ kura ya kupitisha Katiba inayopendekezwa bila ridhaa yake, uongozi wa Bunge Maalumu la Katiba umethibitisha kuwapo kwa dosari hizo.


“Sikuwahi kushiriki kwa namna yoyote ile kwenye kupitisha katiba hiyo. Ukweli ni kwamba nimeumia sana na hadi sasa sielewi hatma ya maisha yangu na usalama wa familia yangu kwa ujumla” alisema Hamis alipozungumza na waandishi wa habari jijini hapa.


Akizungumzia tuhuma hizo za Hamis, Naibu Katibu wa Bunge Maalumu la Katiba, Dk Thomas Kashililah alisema: “Kwa taarifa zetu hakupiga kura siku zote tatu za zoezi hilo. Jina lake katika orodha ya wapiga kura lilikuwa namba 63 na hakupiga kura.”


Alisema hata hivyo wakati wa kuondoa majina ya Wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na wale ambao hawakushiriki jina lake lilisahaulika.


“Tuligundua dosari hiyo na ndiyo maana hatukugawa vitabu siku ya sherehe, tumerekebisha kwa kuchapa vitabu vipya na vitakuwa tayari Jumatano.


“Aidha, majina yanayoonekana katika kitabu ukiacha hilo la Haji lililokosewa majina mengine yapo sawa kwa pande zote mbili na kwamba majina hayo siyo waliopiga kura tu hata wale ambao walishiriki, lakini hawakupata fursa ya kupiga kura majina yao yapo katika kitabu,” alisema Dk Kashililah.


Utata wa kura


Kwa upande wa Zanzibar kura mbili ndizo ambazo zilipitisha Katiba hiyo inayopendekezwa jambo ambalo wadau mbalimbali walihoji namna zilivyopatikana theluthi mbili.


Akitangaza matokeo hayo Oktoba 2, mwaka huu bungeni mjini Dodoma, Dk Kashililah alianza kutoa matokeo ya upande wa Zanzibar ambako wajumbe wengi walikuwa na wasiwasi kuwa huenda usipate akidi ya kura 146 iliyotakiwa.


Kwa jumla, kura za ‘ndiyo’ za Zanzibar zilikuwa ama 147 au 148 na ‘hapana’ ama saba au nane; wakati kwa matokeo ya Tanzania, wajumbe waliopiga kura walikuwa 335 na kura moja tu ndiyo ilikataa ibara zote na kura mbili zilichomoza kukataa baadhi ya ibara.


Akizungumza na gazeti hili jana, Kaimu Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Faustin Sungura alisema, kitendo kilichofanywa na uongozi wa Bunge hilo kinahatarisha usalama wa Hamis.


“Sitta alimkabidhi Rais Kikwete Katiba inayopendekezwa batili kutokana na mchakato wake kugubikwa na utata hususan upatikanaji wa theluthi mbili upande wa Zanzibar, wamepandikiza majina ambayo hayana uhalali kama hili la Hamis walivyomfanyia sasa mpaka hapo tunaendelea kutilia shaka uhalali wa theluthi mbili za Zanzibar. Na kuongeza kuwa; mwananchi

0 comments :

Post a Comment

 

Copyright © 2013. THE WORLD OF TODAY - Haki zote zimehifadhiwa
Template Modify by World of Today TEAM
Proudly powered by Blogger