Dodoma. Siku chache baada ya Bunge la Maalumu la Katiba kumaliza muda wake, matumizi ya fedha zilizobaki kwenye Bunge hilo yameibua mvutano baada ya kuwapo taarifa kuwa fedha hizo ziliisha, huku Wizara ya Fedha ikieleza kuwa bado zipo.
Idadi ya wajumbe wa Bunge hilo kisheria ni 629 na wajumbe ambao hawakuhudhuria vikao vya Bunge hilo tangu Aprili 16, mwaka huu, wanakadiriwa kufikia 140.
Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta, aliwahi kukaririwa akiwaeleza wajumbe wa Bunge hilo kuwa fedha zitakazookolewa zitatafutiwa utaratibu badala ya kurudishwa zilikotoka.
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni, Katibu wa Bunge, Yahaya Khamis Hamad, alisema hakuna pesa zilizobaki na kwamba waliomba Serikali kuwaongezea fedha za siku nne zilizobakia kabla ya kukabidhi Katiba inayopendekezwa kwa Rais Jakaya Kikwete Jumatano wiki hii.
Sitta alipotafutwa kutoa ufafanuzi wake simu yake ilikuwa ikiita bila ya kupokewa kwa muda mrefu.
Alipoulizwa Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba ambaye anakaimu uwaziri wa fedha kuhusu maombi ya nyongeza ya fedha, alisema hajapokea maombi ya nyongeza kutoka katika Bunge hilo na kwamba hawajapata mchanganuo wa fedha walizopewa awali.
“Hatujapata mchanganuo wa fedha zilivyotumika. Utakumbuka kuna wabunge ambao hawakuingia. Kwa hiyo tunaamini kutakuwepo na chenji, kwa sababu haiwezekani kukawa na wajumbe zaidi ya 100 hawakuingia halafu bado fedha ikatumika vilevile,” alisema.
Wabunge wa Bunge hilo walikuwa wakilipwa kwa siku posho ya Sh300,000, kati ya hizo Sh70,000 zilikuwa ni posho za vikao, Sh 230,00 zilikuwa ni fedha za kujikimu.
Mwigulu alisema kuwa Bunge hilo lilipewa bajeti ya Sh32 bilioni na kama Rais Jakaya Kikwete angekubali kuongeza siku 24 zingetumika Sh10 bilioni.
Alisema: “Mimi kwa maoni yangu fedha zote ambazo zitabaki iwe kwenye kura ya maoni ama ingeenda kuwasaidia watoto wa maskini waliokosa mikopo ya elimu ya juu,”alisema.
Alisema katika kipindi cha mwaka jana wanafunzi wenye sifa ya kujiunga na vyuo vikuu wapatao 12,000 walikosa mikopo.
“Chukua taswira ya wale watoto wamesomeshwa na bibi zao na wajane kwa vipesa vya kuokoteza halafu ikafika wakati wa kujiunga na chuo kikuu akakosa fedha ya mkopo tena sio bure bali ni mkopo,” alisema na kuongeza:mwananchi
0 comments :
Post a Comment