Pata Habari Motomoto za Nje na Ndani ya Nchi kwa njia ya E-mail, Andika E-mail yako hapo chini.

Home » » Mwekezaji aliyemzawaida saa Kikwete aibua utata

Mwekezaji aliyemzawaida saa Kikwete aibua utata

Rais Jakaya Kikwete na Robert Shumake

KUMEIBUKA utata kuhusu mfanyabiashara wa Marekani, Robert Shumake, ambaye anakaribia kupewa mradi wa usafiri wa treni kutoka Pugu hadi katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

Mradi huo unaokadiriwa kuwa na thamani ya dola za Marekani milioni 35 (shilingi bilioni 59) umetangazwa na serikali na tayari Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, amesema kama watendaji hawatakuwa magoigoi, unaweza kuanza Desemba mwaka huu.

Hata hivyo, taarifa kutoka Marekani, zinatoa picha tofauti kuhusu tajiri huyu ambaye tayari amekutana na Rais Jakaya Kikwete na kumpa zawadi ya saa aina ya Rolex katika mojawapo ya ziara za Rais nchini Marekani.

Taarifa kutoka Marekani na ambazo tayari zimesambaa katika baadhi ya mitandao ya kijamii zinahoji kama Serikali ya Tanzania ilimchunguza mfanyabiashara huyo anayemiliki Kampuni ya Shumake Global Partners, kabla haijampa shughuli kubwa namna hiyo.

Raia Mwema limearifiwa kwamba Shumake amepata kazi hiyo Tanzania kupitia kampuni ya Shumoja Rail ambayo inaonekana ni mpya na haijawahi kufanya kazi popote duniani.

Baadhi ya Watanzania wamehoji katika mitandao ya kijamii kwamba inakuwaje mfanyabiashara mwenye utata na ambaye ameanzisha kampuni mpya hivi karibuni apewe zabuni ya gharama kubwa kiasi hicho na huku utekelezaji wake ukiwa wa muda mfupi.

Nchini Marekani, Shumake anadaiwa kufisadi fedha za Mifuko ya Hifadhi ya Wastaafu katika mji wa Detroit, baada ya kudaiwa kula njama na baadhi ya wadhamini wa mfuko huo.

Mmoja wa waliokuwa wadhamini wa mfuko na ambaye alihojiwa na mtandao wa Bloomberg wa Marekani, alidai kutiwa shaka na tajiri huyo mwenye asili ya Afrika kutokana na kuwajua hadi kwa majina baadhi ya wadhamini katika mkutano wake wa kwanza kukutana nao.

“Katika masuala ya zabuni, unatakiwa kuwa makini sana na mtu ambaye anamjua kila mtu katika mkutano wenu wa kwanza. Ile pekee ilikuwa ishara tosha kwamba alishakutana nao kabla hata ya kuja kufanya maombi ya zabuni,” alinukuliwa George Orzech ambaye ni mstaafu wa Zimamoto anayewakilisha maslahi yao miongoni mwa wadhamini.

Katika kashfa hiyo ya Detroit, Shumake na wenzake wanadaiwa kuhusika katika matumizi mabaya ya kiasi cha dola milioni 27 za Marekani.

Gazeti hili halijaweza kuthibitisha taarifa kwamba Shumake alikutana na mmoja wa mawaziri wa Kikwete mwaka mmoja uliopita.

Taarifa kutoka katika mtandao wa Amazon, zinamueleza Shumake kama mjasiriamali wa biashara ya uuzaji wa viwanja na nyumba (Real Estate) ambavyo vina thamani ya dola bilioni moja.

Shumake pia ni Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Marekani lakini pia taarifa nyingine zinaeleza kuwa pia ni Balozi wa Heshima wa Botswana nchini Marekani pia.

Juhudi za kumpata Waziri Mwakyembe kueleza endapo serikali ilifanya utafiti wa kutosha kwenye mazungumzo yake na Shumake zilishindikana kwa vile yuko nje ya nchi kikazi na hadi tunakwenda mitamboni alikuwa hajajibu maswali aliyotumiwa na gazeti hili kwa njia ya barua pepe.

Hata hivyo, mmoja wa maofisa wa ngazi za juu wa Wizara ya Uchukuzi aliyezungumza na Raia Mwema kwa masharti ya kutotajwa jina, alisema serikali haitapata hasara yoyote kutokana na uwekezaji wa Shumake.

Zabuni ilikuwa haina sababu katika mradi huu kwa sababu serikali haitoi fedha yoyote. Hakuna hasara. Huu si sawa na Mradi wa Mabasi Yaendayo Kasi (DART) ambao serikali imeingia gharama.

“Kuna miradi mingine serikali inatafuta wawekezaji lakini yenyewe haiwezi kuwekeza. Akijitokeza mwekezaji ambaye yuko tayari anapewa mradi. Mfano ni mradi wa kuzalisha umeme wa Stiegler’s Gorge… Akijitokeza mtu kutaka kuuendeleza, atapewa na serikali bila zabuni,” alisema ofisa huyo wa serikali.

Taarifa kutoka mitandaoni zinaeleza pia kwamba Shumake amewahi kutangazwa kufilisika katika miaka ya nyuma

0 comments :

Post a Comment

Copyright © 2013. THE WORLD OF TODAY - Haki zote zimehifadhiwa
Template Modify by World of Today TEAM
Proudly powered by Blogger