Pata Habari Motomoto za Nje na Ndani ya Nchi kwa njia ya E-mail, Andika E-mail yako hapo chini.


Home » » CCM, Ukawa FULL matokeo, SOMA HAPA CCM ILIVYO CHAKAZWA

CCM, Ukawa FULL matokeo, SOMA HAPA CCM ILIVYO CHAKAZWA


Mawakala wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wakihesabu kura za Mtaa wa Kambarage Kata ya Igogo Mwanza jana. Picha na

Kilimanjaro


Katika Kitongoji cha Njiapanda Magharibi (Vunjo) CCM ilishinda kwa kura (343), NCCR-Mageuzi (195) na TLP-(36).


Katika Kitongoji cha Njiapanda Mashariki (Vunjo), NCCR-Mageuzi imeshinda kwa kura (277), CCM (239), Chadema (71) na TLP (37). Katika Kitongoji cha Faru (Vunjo) Chadema imeshinda kwa kura (288), CCM (93), TLP (27) na NCCR-Mageuzi (7). Katika Kitongoji cha Darajani (Vunjo), NCCR-Mageuzi imeshinda (208), CCM (204), Chadema(169) na TLP (46). Kitongoji cha Kashinda (Vunjo), NCCR-Mageuzi imeshinda kwa kura 31, CCM (19) na Chadema (13). Kitongoji cha Makere NCCR-Mageuzi imeshinda kwa kura 52, CCM (20). Kitongoji cha Ofisini Chadema imeshinda kwa kura 43, NCCR-Mageuzi (20) na CCM (12).


Katika Kijiji cha Marawe Kirua (Vunjo), CCM imeshinda kwa kura 164, Chadema (77), NCCR-Mageuzi (84) na TLP (43). Katika Manispaa ya Moshi Mtaa wa Rengua, Chadema imeshinda kwa kura 83 na CCM (58). Mtaa wa Bonitte, Chadema imeshinda kwa kura 65 na CCM (51). Mtaa wa Kiusa CCM imeshinda kwa kura 143 na Chadema (95). Mtaa wa Korongoni Chadema imeshinda kwa kura 252 na CCM (244). Mtaa wa Sabasaba CCM imeshinda kwa kura 228, Chadema (114) na katika Mtaa wa Kambaita CCM ilishinda kwa kura 172 na Chadema(171).





Kilindi


CCM imepita bila kupingwa katika vitongoji 615 na vijiji 102. Msimamizi wa Uchaguzi wa Wilaya ya Kilindi, Daudi Maige alisema jana kuwa kutokana na CCM kupita bila kupingwa katika vijiji 102 na vitongoji 615 uchaguzi ulilazimika kufanyika katika vijiji viwili tu, Kileguru na Makasini.





Mbeya


Mtaa wa Sabasaba nafasi ya Mwenyekiti CCM, Aidan Ng’oma, kura 74 wakati Anna Mwenda wa Chadema akipata kura 23. Mtaa wa Kisoki mgombea wa uenyekiti Edward Mwakasiti wa CCM alitangazwa mshindi baada ya kupita bila kupingwa.


Katika Mtaa wa Mwasyoke, uchaguzi wa mwenyekiti uliahirishwa, lakini kwa upande wa wajumbe, CCM ilipata viti vitatu wakati Chadema ilipata viwili. Mtaa wa Itezi, mgombea wa CCM, Anania Sanga alipita bila kupingwa, kama ilivyokuwa kwa Daud Kipenya wa chama hicho kwa Mtaa wa RRM. Kutoka Vwawa mgombea wa uenyekiti Kitongoji cha Masaki (Chadema) alipata kura 96 wakati CCM ilipata kura 48 BOFYA HAPA KUENDELEA

0 comments :

Post a Comment

 

Copyright © 2013. THE WORLD OF TODAY - Haki zote zimehifadhiwa
Template Modify by World of Today TEAM
Proudly powered by Blogger