Wananchi wamsimika ‘mwenyekiti’ wao kibabe
Dar/ mikoani. Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika jana nchini, ulitawaliwa na vituko katika sehemu nyingi, lakini kikubwa ni kile kilichotokea katika Kijiji cha Kambi ya Chokaa, Wilaya ya Simanjiro, mkoani Manyara baada ya wananchi kumweka madarakani na kumwingiza ofisini Joshua Kuney (CCM) kuwa mwenyekiti wa kijiji hicho, badala ya Mbuki Mollel aliyeteuliwa na chama hicho kuwania nafasi hiyo.
Pamoja na hatua hiyo, wananchi hao pia
waliwapitisha kwa kauli moja bila kupiga kura wajumbe wote wa serikali
ya kijiji kupitia CCM kutokana na kijiji hicho kutokuwa na wagombea
kutoka vyama vya upinzani.
Kabla ya kumpeleka ofisi ya kijiji na kumsimika
kuwa mwenyekiti, wananchi hao walimzungusha Kuney kwa maandamano ya
amani wakiwa wamembeba juujuu na kuhitimisha kwa kumbariki kwa mila za
Kimasai kwa kumwagia maziwa mwili mzima, ikiwa ni ishara ya baraka.
Tukio hilo linakwenda kinyume na uamuzi wa vikao
vya CCM wilaya ya Simanjiro ambavyo vilimwengua Kuney ambaye alikuwa
ameshinda kwa kura 335 dhidi ya 215 za Mollel wakati wa kura za maoni.
Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, Letee Sailepu
ambaye hakugombea tena nafasi hiyo, alisema wakazi wa kijiji hicho
hawako tayari kuongozwa na mtu wasiyemtaka.
“Mwenyekiti wa kijiji ni kiongozi wa watu
anayestahili kukubalika kwa wananchi anaowaongoza. Joshua ndiye
mwenyekiti wetu na hatutabadili msimamo katika hili,” alisema Sailepu.
Akizungumza muda mfupi baada ya matukio hayo,
Kuney aliahidi kuongoza kwa haki na kuwaunganisha wananchi wote wa
kijiji hicho ili kujiletea maendeleo.
“Sauti ya watu ni sauti ya Mungu. Sina budi
kuitikia wito wa wananchi wa kuwa kiongozi wao. Nitaongoza kwa kufuata
sheria, kanuni na taratibu kwa faida na masilahi ya wananchi wenyewe,”
alisema Kuney.
Kwa upande, mgombea aliyepitishwa na CCM, lakini
akakataliwa na wananchi, Mbuki Mollel alisisitiza kuwa yeye ndiye
mwenyekiti halali kisheria na ataongoza kwa kutumia busara ili
kuwaunganisha wananchi wote, wakiwamo wanaompinga.
Diwani wa kata ya Naisinyai, kilipo Kijiji cha
Kambi ya Chokaa, Kilempu Ole Kinoka aliunga mkono uamuzi wa wananchi
kumweka madarakani mtu wanayemtaka kuwa mwenyekiti wao kwa sababu ndiyo
wenye uamuzi wa mwisho.
Katibu wa CCM Mkoa wa Manyara, Ndeng’aso Ndekubari
alisema amepata taarifa ya msimamo wa wananchi na kuahidi kuwa chama
hicho kitatoa uamuzi baadaye.
Katika tukio jingine, zaidi ya wapigakura 200 wa
Kitongoji cha Nanja Madukani, Kata ya Lepurko, Monduli mkoani Arusha
walishindwa kupiga kura baada ya kituo hicho kukutwa kimefungwa na
kuwekwa tangazo la kutokuwapo kwa uchaguzi kwa maelezo kuwa mgombea wa
CCM amepita bila kupingwa, huku kukiwa na madai kwamba haikuwa kweli ENDELEA KWA KUBOFYA HAPA
0 comments :
Post a Comment