Pata Habari Motomoto za Nje na Ndani ya Nchi kwa njia ya E-mail, Andika E-mail yako hapo chini.


Home » » FAIDA NA HASARA YA LIKIZO NA MUONGOZO WAKE

FAIDA NA HASARA YA LIKIZO NA MUONGOZO WAKE


http://www.indian-ocean.com/wp-content/uploads/2014/04/A-family-on-holiday-in-th-014.jpg
ITAKUMBUKWA kuwa mada hii tulianza nayo wiki iliyopita ambapo tulitazama baadhi ya dokezo muhimu za kuzingatia kwenye likizo, na mwisho tukakomea kwenye kifungu hiki:

Mwanafunzi wangu, naamini utakuwa na swali juu ya mada hii: “Nifanye nini katika kipindi cha likizo ili nipate faida zote mbili?” Jibu liko kwenye vidokezo vitatu, KWANZA ni kwako mwanafunzi kujitambua, PILI kwa mwalimu wako na TATU kwa wazazi.

Leo tuanze kwa kuchambua vidokezo vitatu kama ifuatavyo! KWANZA: Ninaposema mwanafuzni kujitambua nina maanisha kuujua uwezo wake wa kimasomo na udhaifu binafsi.

Uumbwaji hutofautiana kati ya mtu na mtu, kuna wengine uelewa wao ni mkubwa na hata kumbukumbu zao ni za hali ya juu. Hawa huwa hawahitaji kujikumbusha vitu mara kwa mara, lakini wengine ni dhaifu katika mambo niliyotaja, njia pekee ya kujiweka sawa ni kujikumbusha kila mara.

Nikisema hivyo naweka mkazo kuwa kipindi cha likizo siyo kipindi cha kuweka kando masomo na kucheza, bali ni cha kuendelea kupanua uelewa kwa kuchambua kwa kina yale yote uliyojifunza shuleni.

Msisitizo wangu ni kupitia notisi na kujifunza kwa vitendo, nikiwa na maana hata matembezi yasiwe ya kihuni bali ya kujifunza zaidi. Mfano kutembelea makumbusho ya taifa na hata mbuga za wanyama, viwanda na kujionea mila na tamaduni tofauti.

PILI: Mwalimu anayejali mafanikio ya wanafunzi wake lazima awawekee mazingira ya kujisomea wakati wa likizo, hiyo inaweza kuwa ni kuwapa kazi za kufanya wakiwa nyumbani au kuwaandaa kisaikolojia inaweza kuwa ni kauli ya kuwataka wasome topiki fulani kutokana na kusudio la kufanya mtihani mara baada ya kutoka likizo. Hiyo itawahamasisha wanafunzi kujisomea.

TATU: Pamoja na kuwa wazazi wengi siyo washirika wazuri wa elimu ya watoto kwa maana ya kutojua namna ya kuwasaidia kimasomo, bado wazazi wana jukumu la kuwahamasisha watoto wao wajisomee kipindi cha likizo. Inaweza kuwa ni kuwalipia masomo ya ziada au kuwatengea muda mahususi wa kujisomea. Naamini nimeeleweka; nakutakia likizo njema. global publisher

0 comments :

Post a Comment

 

Copyright © 2013. THE WORLD OF TODAY - Haki zote zimehifadhiwa
Template Modify by World of Today TEAM
Proudly powered by Blogger