Pata Habari Motomoto za Nje na Ndani ya Nchi kwa njia ya E-mail, Andika E-mail yako hapo chini.


Home » » LA VEDA: IDRIS, FEZZA KESSY NA DIAMOND WAMETOA GUNDU KWA WASANII WA BONGOA

LA VEDA: IDRIS, FEZZA KESSY NA DIAMOND WAMETOA GUNDU KWA WASANII WA BONGOA



La Veda baada ya kuwasili jijini Dar akitokea nchini Afrika Kusini alipokwenda kushiriki fainali za BBA.



La Veda akipokelewa baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.





La Veda akipozi na baadhi ya wadau waliofika kumpokea.

MWANADADA, aliyeiwakilisha Tanzania katika shindano la Big Brother Hotshots, Irene Neema Vedastous ‘LA VEDA' amefunguka kuwa Diamond, Fezza na Idris wameondoa gundu kwa ushindi wao.

Akizungumza na GPL leo jioni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, wakati akiwasili kutoka Afrika ya Kusini alipokwenda kuungana na washiriki wengine wa BBA katika fainali, La Veda alisema,

“Binafsi nimefurahi sana kwa Idris kushinda Dola za Kimarekani 300,000, ni furaha kubwa sana kwangu na kwa Watanzania kwani naamini pia Diamond kuchukua tuzo tatu za Channel O na nyingine aliyopata juzi kutoka Nigeria, Fezza kuingia tena mjengoni wote watakuwa wameondoa gundu kwa wasanii wa Kitanzania’, alisema.

Aidha La veda amewaomba Watanzani kujitokeza kwa wingi kumpokea Idris siku atakapowasili maana ushindi wake unazidi kuiweka Tanzania katika ramani nzuri kimataifa.global publishers

0 comments :

Post a Comment

 

Copyright © 2013. THE WORLD OF TODAY - Haki zote zimehifadhiwa
Template Modify by World of Today TEAM
Proudly powered by Blogger