Pata Habari Motomoto za Nje na Ndani ya Nchi kwa njia ya E-mail, Andika E-mail yako hapo chini.


Home » » Filamu ya ‘Nimekubali Kuolewa’ ya Dr Cheni yaruhusiwa kutoka

Filamu ya ‘Nimekubali Kuolewa’ ya Dr Cheni yaruhusiwa kutoka

Msanii wa filamu, Mahsein Awadh Said aka Dr. Cheni’ amesema filamu yake ya ‘Nimekubali Kuolewa’ iliyokuwa imezuiwa kutoka na Bodi ya Filamu Tanzania (TFB) inatarajiwa kutoka mapema mwakani baada kukamilisha matakwa yao.

Dokta Cheni alisema kuzuiliwa kwa filamu hiyo kulimnyima raha kiasi cha kumfanya asifanye kazi nyingine mpaka akamilishe kazi hiyo.


“Nimefanikiwa kuipigania filamu yangu ya ‘Nimekubali Kuolewa’, itatoka mwezi wa pili mwakani. Kikubwa nilichokifanya ni kurekebisha baadhi ya vitu ambavyo walihitaji na imekamilika kwahiyo watu wakae mkao wa kula tu,” alisema Cheni.

0 comments :

Post a Comment

 

Copyright © 2013. THE WORLD OF TODAY - Haki zote zimehifadhiwa
Template Modify by World of Today TEAM
Proudly powered by Blogger