Mwanamuziki Judith Wambura 'Lady Jaydee'
Lady Jaydee akisoma gazeti la Staa Spoti.
Mhariri Msaidizi wa Gazeti la Jambo Leo, Frank Balile (kulia), akimuelekeza jambo Lady Jaydee wakati akimuonesha gazeti hilo.
Mwanadada
anayefanya vizuri katika muziki wa kizazi kipya nchini, Judith Wambura
'Lady Jaydee' akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa gazeti la Jambo Leo,
alipotembelea chumba cha habari Dar es Salaam jana.
Dar es Salaam, Tanzania
MWANADADA
anayefanya vizuri katika muziki wa kizazi kipya nchini, Judith Wambura
'Lady Jaydee' amesema kamwe atarajii kujiingiza katika masula ya siasa
kama wanavyofanya wanamuziki wenzake.
Kauli
hiyo aliitoa wakati akizungumza na waandishi wa habari wa gazeti la
Jambo Leo Dar es Salaam jana, baada ya kutembelea chumba cha habari cha
gazeti hilo katika Jengo la Hifadhi House katika makutano ya Barabara za
Azikiwe na Samora.
"Binafsi
sitarajii kuingia katika masula ya siasa mimi nitaendelea na muziki na
hao wenzangu waliojiingiza katika siasa ni utashi wao.
Alisema
anafurahi kufanya mziki na wala hajuti kwa kuwa unamuongezea kipato
kikubwa ni kutunga nyimbo zenye mahudhui na mvuto na kwa wakati husika.
Baadhi
ya wanamuziki waliojiingiza katika siasa ni Joseph Mbilinyi 'Sugu'
ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), Joseph Haule 'Profesa J, Khadija Shabani 'Keisha'
Ummy Wenslaus 'Dokii, na wengine kama Fullgence 'Mwanacotide' ambaye
yupo Chadema. CHANZO CCM BLOG
0 comments :
Post a Comment