Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)
MAANDALIZI ya siku ya uhuru wa Tanganyika (Tanzania
Bara) Desemba 9, kutimiza miaka 53, yanaendelea Uwanja wa Uhuru ambapo
kutakuwa na gwaride la kijeshi vikundi vya sanaa, kwaya, halaiki ya
vijana, ‘brass band’ na matarumbeta.Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki, amesema milango katika Uwanja wa Uhuru itakuwa wazi kuanzia saa 12:00 asubuhi ambapo wananchi watakaofika katika hafla hiyo watatumia mlango wa kusini upande wa Barabara ya Mandela kuingia uwanjani, na waalikwa wenye kadi watatumoa mlango wa geti namba mbili 2 na viongozi watatumia geti namba tatu 3.
0 comments :
Post a Comment