Wiki jana kuna Waziri maarufu wa zamani, alifanya kioja.
Mstahiwa alikuwa akitoka hafla fulani ya hali ya juu, mitaa ya kitajiri
tajiri, London na mkewe. Wameshachapa maji sawasawa; wakasimamisha
teksi. Sasa kwa vile dereva alikuwa akichukua njia za mikato kukwepa
misongamano ya magari, bwana mkubwa akaanza kumkaripia. Makaripio
yakaishia kuwa ugomvi na matusi juu. Dereva kuona anatukanwa, akaanza,
kisiri siri, (bila bwana mkubwa kung’amua ) kunasa mazungumzo katika
simu yake. Akapeleka vioja katika gazeti kubwa la hapa Uingereza. Neno
kwa neno likachapwa. Habari zikaenea kama utitiri.
Waziri Mstaafu aliona aibu ikambidi aombe radhi, wazi wazi.
Matusi Mheshimiwa David Mellor aliyomrushia dereva
teksi ambaye hadi tukio hili linapoandikwa hajatajwa jina kwa kuhofia
asijefikwa ( si Afrika tu ambapo viongozi wana uwezo wa kumhasimu mlala
hoi aliyewaudhi!) na mabaya. Na yote yaliandikwa. Usichezee vyombo vya
habari, Uzunguni. Na gazeti hili, si la umbea. Maana ingekuwa kwetu
Afrika labda magazeti ya udaku tu ndiyo yangetangaza, mambo yaishie
vichochoroni. Hili ni gazeti linalosomwa na asilimia kubwa ya
Waingereza.
Daily Mail. Huwa haliweki picha za wanawake wakiwa uchi au uhuni na mabezo. Hapana.
Kiini cha matusi yake mstahiwa Waziri mstaafu ni matabaka.
Akajitutumua zamani alikuwa Waziri serikalini.
Pili, kitaaluma amezawadiwa tuzo kutokana na kazi yake ya utangazaji
redioni. Tatu, anajuana na kuaminika na mtukufu Malkia Elizabeth; ni
miongoni mwa wanasheria maalumu walioteuliwa kusimamia na kuhukumu kesi
kubwa kubwa. Hii desturi ya kizamani sana katika himaya ya Waingereza
yenye kanuni za kimwinyi kutokana na hulka, mavazi, kazi na nafasi.
Sasa alipopandwa ghadhabu katika teksi, Mellor
alijigamba yeye ni vitu vyote hivyo na kumtaka jamaa afunge mdomo kila
alipomjibu. “Sina haja ya kukufahamu wewe nani. Hujui lolote kuhusu
London.” Juu yake akijazia matusi na dharau za kisultani.
Baada ya kitambo kidogo, dereva akajibu hapendi
kuamrishwa. Kaifanya kazi ya teksi miaka kumi. Kwamba Mstahiwa asijaribu
kumtisha.
Mstahiwa akachachamaa. “Umeendesha teksi miaka
kumi. Mimi nimeishi mji huu miaka 40. Nilikuwa waziri na nilishafanya
kazi rasmi teule ya malkia miaka tele. Funga mdomo. Endesha tu gari....”
Hivyo ndivyo mgogoro ulivyoendelea na kadri jamaa
walivyoendelea kujibishana dereva teksi akawa sasa hasemi sana ila
kurekodi mazungumzo. Hapo sasa Waziri mstaafu akikazania na kuhimiza
alivyo muhimu na mashuhuri. Kwamba anaweza kufanya kampeni hiki kigari
chake mwananchi kisiwe tena barabarani. Kwamba atamsema katika redio.
Sasa. Hilo moja.
Hapa Uingereza jambo kama hili linapobainika na kusambaa huwa haliishi
0 comments :
Post a Comment