Sumbawanga. Watu wasiofahamika wamemuua mkazi wa Kijiji cha Vikonge Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi, Kitola Jeremia (45) kwa kumkatwa mapanga sehemu za mwili wake sambamba na kumtoboa tumbo .
Watu hao wanadaiwa kutenda unyama huo juzi saa mbili usiku nyumbani kwa marehemu alikokuwa akiishi kijini hapo na familia yake.
Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari alisema siku ya tukio marehemu alikuwa nje ya nyumba yake na mkewe Yulitha Stephano (34) pamoja na wasaidizi wao wa kazi wakipata chakula cha usiku na mara ilitokea pikipiki iliyobeba watu wawili waliokuwa wamevaa makoti meusi.
Imedaiwa walipofika walimsalimiana marehemu na kumweleza kuwa wametokea Kijiji cha Mishamo lakini wanaishi Kijiji cha Kakese na kwamba wanatafuta eneo la kuchungia mifugo yao na marehemu aliwajibu maeneo yanapatikana hivyo walale ili siku inayofuata awapeleke kwa mwenyeji anayeweza kuwapatia eneo.
Inasemekana baada ya mazungumzo hayo wageni hao waliomba chakula na sehemu ya kulala, walitimiziwa baadaye kuonyeshwa sehemu ya kulala. Kwa mujibu wa Kamanda watu hao waliamka na kwenda kwenye nyumba aliyokuwa amelala Jeremia na mkewe, walivunja mlango na kuingia ndani na kuanza kumshambulia marehemu kwa mapanga.
Kamanda huyo alisema mkewe alipoona mumewe anashambuliwa alianza kupiga mayowe ya kuomba msaada hata hivyo wauaji hao walianza kumshambulia na yeye na kumjeruhi kichwani.
Alisema mke wa marehemu alifanikiwa kukimbia hadi kwenye nyumba jirani ya wasaidizi wa kazi na kuwaeleza kilichotokea.
Wasaidizi hao walipofika kutoa msaada walimkuta marehemu tayari ameshafariki na wauaji wakiwa wametokomea kusikojulikana. Alieleza kuwa uchunguzi wa awali unaonyesha chanzo cha mauaji hayo ni ugomvi wa mali kati ya marehemu na familia ya mkewe mkubwa. chnzo mwananchi
0 comments :
Post a Comment